Francia A.
Camera imeshasimama tayar kwenye mti wake wa chuma. Fundi wenu japo alichelewa kufika ila amefanya kaz nzur ya kunifungia. Sasa ntaweza kuona kwa upana zaidi ya kile kinachoendelea mlangoni mwa nyumba na hata kwa pembeni kwenye fensi.
Christian M.
Kazi imeanza ya kufunga hii Camera.Hapa kilichobaki ni kuipachika tu ukutani.Kuunganisha na simu nimeweza na imenichukua muda mfupi sana. Hii lazima niifunge leo leo ili nione kila kinachoendelea kwenye saiti yangu huko magwepande.
Gaudensia M.
Nimeichukulia hapa Moshi kwa wakala wenu mwenye duka la simu. Kashanipa maelekezo ya namna ya kuitumia.Mmekua waaminifu kwa kunipa camera nliyochagua na pia camera ina ubora mzuri.Asanteni
Berkant A.
Good service! Delivery was quick to my office. I have already tested it and seen the video and audio quality. I appreciate the professionalism you have shown in handling my order.The delivery guy knew how to speak English, which was a surprise to me as i needed no one to translate for me.
Shamte M.
Camera imeshanifikia hapa ofisini kwangu Kibo complex. Delivery wenu abdallah alinifanyia delivery leo mchana. Baadae ntasajili laini ili niweze kuona matukio live kupitia simu yangu. Ntaenda kuifunga hii camera nyumbani kwangu kesho Mungu akipenda.
Benedict f.
Tupo kwenye process ya kuinganisha na kuifunga hii camera na fundi hapa Iringa. Imetufikia salama kupitia wakala wenu hapa mjini.Mimi saiti yangu ipo ipogolo hapa. Wenzangu wameiona na kuipenda pia, watawatafuta. Nimeshawapa no zenu
Amos N.
Leo tupo saiti tunafunga hii camera yenu mliotuuzia.Nimeshaiunganisha na simu yangu, naona vizuri kwa simu yangu na mke wangu pia anaona kwa simu yake. Hii itaongeza ulinzi kwenye shamba letu. Kumekua kuna matukio mengi sana ya wizi.
Sadock M.
Camera ameifunga fund wenu hapa nyumbani kwangu kinondoni. Ameshanielekeza namna ya kuitumia.Nimeipenda zaidi hii camera baada ya kujua kwamba tunaweza kuona zaidi ya simu moja, kila kinachoendelea hata tukiwa mbali na eneo la tukio.
Ashraf H.
sasa hivi naona kila mtu anayeingia na kutoka bila shida yoyote.Nimeongeza nyingine tena ili niweze kua na ulinzi zaidi nyumban kwangu.Kwanza sikuamin kama ingenifikia huku Kigoma.Mmekua waaminifu na kunitumia had huku.Asanteni sana