Mustapha A.
Nje kwa nyumba yangu nimeamua niongeze camera nyingine.Hua nasafiri mara kwa mara kwenda Dodoma kikaz.Hizi camera zitanifanya nione kwa usahihi mambo yanayoendelea nyuma yangu.Hivi karibuni ntafika dukani kuona bidhaa zingine
Danstan J.
Nimefunga karibu na nje na pia nyuma ya nyumba.Tangu nimefunga nimeweza kushuhudia mengi yanayoendelea hapa kwangu.Hizi camera zitaendelea kunisaidia kujua kila kitu kinachoendelea.Malalamiko yangu naombeni mlete tena memory card za 128GB ili tununue full package kutoka kwenu.
Innocent S.
Matukio nayaona vizuri kupitia simu yangu.Nimefurah namna inavyofanya kaz haswa usiku inavyoona vizuri watu.Ntaongeza nyingine kwa ajili ya site zangu za dodoma.
Joash J.
Nimefunga kwenye banda langu la mifugo ili nione vizuri usiku.Wizi umekua mkubwa sana kwenye maeneo nnapokaa.Hii camera itanifanya nijue nani hua ananichezea michezo na mifugo yangu haswa kipind cha usiku
Zarina M.
Shambani kwangu pamekua na uangalizi mzuri sasa hivi.Naona kila kitu kinachoendelea. Vijana wangu kuna muda wanahitaji usimamizi mkali ili kuondoa uzembe na udanganifu unaoweza kutokea. Huduma yenu ni nzuri na nimeipenda. Ntawaletea na wateja wengi watakavyoiona hii ya kwangu
Mahmood J.
Nimepokea tayari hapa Arusha mitaa ya sakina. Wakala wenu alinikabidh hio camera. Ntaifunga kesho ili niweze kuona kinachoendelea nyumbani kwangu pindi nkitoka.
Frank B.
Sasa hivi ulinzi kwenye go down langu ni mzuri.Naweza kuona kila kitu kinachoendelea yaani.Nimefurahi sana.Ntaongeza zingine ili nifunge kule nyuma pia.Nataka kujua kila kitu kinachoendelea kwenye ofis yangu
Athanas M.
Nafanya testing hapa nje ya duka langu.nkifanikiwa kufunga ntawaambia. Nataka kuendelea kuona matukio ya duka hata nkiwa nyumbani au nje ya mkoa wangu wa Morogoro. Line ya simu tayari nimeshasajili kwa ajili ya kuweka kweny camera
Shadrack M.
Camera imefika salama salmin hapa Iringa mjini.Najivunia kua mteja wenu na huu ni mwaka wa pili sasa.Bidhaa zenu hazijawah kunipa changamoto kubwa sana ya kunifanya niwahame.Nawaomba msiingiwe na tamaa na kuanza kuleta bidhaa zisizo na ubora ili kutengeneza faida zaidi.
Robertson M.
Mzigo umeshawasili nyumbani kwangu Shinyanga.Wakala wenu aliwahi kunipigia kabla hata mzigo haujanifikia.Ntatoa mrejesho zaidi baada ya kuzifunga.Week ijayo tegemea mrejesho mwingine kutoka kwangu
Adelina M.
Nlikua nahitaji kujua na kuwatambua wote wanaopita kutoka getini ndo maana nimeifunga ukutani ili ulinzi wa nyumba uimarike.Ntaongeza nyingine nje ya geti niweze kua naona maeneo mengi ya nyumba yalio muhimu.
Davis r.
Nimefungua kila kitu kwa uangalifu kabla ya kuifunga.Nimeshapokea maelekezo yenu kwa video ya namna ya kufunga.Nimeipokea bidhaa yenu nkiwa bukoba kutoka kwa wakala wenu
Hidaya m.
Camera imefika salama kabisa.Nitaifunga kesho mchana.Nimeona tayari mmenitumia maelekezo ya namna ya kuitumia.Huduma ni nzuri.Nitaongeza nyingine wiki ijayo nkaifunge kweny ofis yangu nje.Kitu ambacho sijakipenda ni watu wenu wa usafiri.Hawanikupigia mapema nikachukue mzigo badala yake ikabidi niufate kesho yake.Zaidi ya hapo mpo vizuri Almasishop.
Robert C.
Nimefungua huu mzigo.Naona camera imekamilika na vifaa vyake vyote.Nililipa kabla hamjanitumia huku Mara.Kiukweli nliogopa kidogo wakati nafanya malipo kwani mitandaoni matapeli wengi.Rafiki wangu ashawahi tapeliwa.Ila kwa uaminifu mlionionesha huu, ntaagiza bidhaa zenu tena
Wambura D.
Nilichukua kwa wakala wenu wa mwanza pale nata.Mi ni mkazi wa Simiyu.Nimefanikiwa kuifunga vizur iangalie matukio yanayoendelea hapa nyumbani kwangu.Ntawaletea wateja wengi kutoka huku kwetu
Edgar M.
Nlipokea camera pale sakina arusha kwa wakala wenu.Kwenye kufunga haikuleta shida.Kabla hamjanitumia video ya maelekezo nlitaka kufunga mwenyewe nikashindwa kwasababu maandishi ya kwenye kitabu cha maelezo ni madogo kwangu kusoma.Mimi ni mbovu wa kusoma mandishi madogo kwasababu ya uzee.
Nickson S.
Ulinzi umeimarika hapa site kwa kufunga camera. Imenichukua muda mfupi kuunganisha na simu.Site yangu haina umeme wa Tanesco ndo maana imebid nifunge camera ya solar ili niweze kuona vyote vinavyoendelea usiku na mchana.
Kassim M.
Nimeileta huku shambani kwangu nifunge leo leo kabisa.Nmechoka kuibiwa usiku mifugo .Kila baada ya siku kadhaa kuna matukio ya wizi yanatokea.Nataka kuongeza ulinzi niweze kufahamu nini kinaendelea shambani kwangu.Nlichukulia pale mbeya mjini